Jamii Iwekeze Kwa Wanawake Walemavu Na Watoto Kupunguza Maambukizi Ya Virusi Vya Corona Nchini

Shirika lisilo la kiserikali limeanzisha campaign ya kuhamasisha jamii ili kusaidia wanawake wenye ulemavu na watoto wa kike katika kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19.

Mkrugenzi wa Peace Life For People Disability Foundation, Sophia Mbeyela amesema wameanzisha kampeni inayoitwa “Tusimame Nao” ili jamii ijitokokeze kuchangia chochote na kuwapa mahitaji maalumu.

“Mara nyingi janga lolote lina potokea nchini au nchi nyingine wanawake na watoto wanaathirika sana naomba tusimame pamoja nao katika kipindi hiki cha Corona kwa changia kitu chochote,” amesema.

Anasema jamii isimuache mtoto wa kike wala mlemavu katika kipindi hiki cha ugonjwa hatari. “Kuna familia nyingi za watu wenye mahitaji maalumu. Katika kundi hili wanakosa hata sabuni ambayo wewe unayo. Hakuna mwingine wa kuwasaidia ila ni jukumu langu mimi na wewe tuungane pamoja katika hili mchango wako utaokoa maisha ya  wengine. Jilinde na uwalinde wengine”, amesema.

Imeandikwa na Hellen Nachilongo, (23 April 2020) – Dar es Salaam

Translate »